17 Desemba 2014 - 20:32
Netanyahu aomba Hamas irejeshwe kwenye orodha ya magaidi

Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu ameutaka Umoja wa Ulaya kulirejesha haraka kundi la Hamas katika orodha ya makundi ya kigaidi.

Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu ameutaka Umoja wa Ulaya kulirejesha haraka kundi la Hamas katika orodha ya makundi ya kigaidi.

Kauli hiyo ameitoa leo baada ya mahakama ya Ulaya kuamuru kundi hilo lenye itikadi kali za Kiislamu la Palestina, kuondolewa kwenye orodha hiyo. Netanyahu amesema hawajaridhishwa na hatua hiyo na kwamba wanatarajia Ulaya italirejesha kundi hilo kwenye orodha ya magaidi. Hata hivyo, uamuzi huo umepokewa kwa furaha na Hamas na wameipongeza mahakama hiyo kwa uamuzi iliouita ''hatua nzuri''.  Msemaji wa Hamas, Fawzi Barhum amesema huo ni ushindi kwa Palestina na haki ya watu wao. Mahakama Kuu ya Umoja wa Ulaya imesema uamuzi wa kuiondoa Hamas kwenye orodha hiyo, umezingatia misingi ya kiufundi. Hamas ambayo iliorodheshwa mwaka 2001 kama kundi la kigaidi, imekuwa ikitawala katika Ukanda wa Gaza tangu mwaka 2007.

Hamas ni kundi la wanamgambo wa kipalestina ambao walikataa dhuluma za Israel na kuapa kuwa watapambana kutafuta haki zao, kwani Israel imechukua ardhi yao kwa nguvu, Israel imefanya mauaji yasiyokuwa na mfano dhidi ya raia madhulumu wa ukanda wa Gaza, na kuua maelfu ya watu ambapo wengi wao ni wanawake na watoto.

Kitendo cha bunge la Ulaya kuitoa Hamas katika makundi ya kigaidi ni kitendo sahihi na kitendo cha kuwaweka kwenye orodha ya magaidi hakikuwa sahihi tangu awali, kwani Hamas na hata Hizbollah si makundi ya kufanya hujuma kwa watu wasio kuwa na hatia, bali makundi haya yanapambana na serikali ya Israel ili kurudisha haki zao walizodhulumiwa na Israel, Je kupigania haki yako ni Ugaidi? Hili ni swali ambalo serikali ya Israel inatakiwa ilijibu kinaga ubaga.

Kitendo cha Hamas kuondolewa kwenye orodha ya magaidi kulipa uhuru kundi hilo kufanya biashara na harakati zake bila vikwazo, kitu ambacho kinalitia hofu taifa la Israel.  

 

Tags